Dar es Salaam. Licha ya kutangaza kuachana na muziki. Mwanamuziki Vanessa Mdee ni miongoni mwa wasanii waliowahi kuupambania muziki wa Bongo Fleva kutambulika kimataifa.

Miaka saba iliyopita Vanessa alikuwa miongoni mwa wasanii walioteuliwa kuimba wimbo wa “Vaishnav Jan To” katika maadhimisho ya miaka 150 ya kuzaliwa kwa Mahatma Gandhi, ambaye ni baba wa taifa wa India.

Mradi huo wa Kimataifa uliofanyika mwaka 2018, ulihusisha wasanii kutoka nchi mbalimbali. Kila mmoja akiimba sehemu ya wimbo huo maarufu ambao Gandhi aliupenda wimbo unaohamasisha utu, usawa na huruma.

Kwa mujibu wa taarifa za Ubalozi wa India, Vanessa alichaguliwa kuwakilisha Tanzania kutokana na mchango wake katika kukuza muziki wa Afrika Mashariki na uwezo wake wa kutumia Kiswahili kwa ufasaha. Ambapo hatua hiyo ilimpa mafanikio makubwa mwaka 2019 alitunukiwa tuzo ya heshima na Waziri wa Mambo ya Nje wa India. 

Aidha mbali na Mdee mradi huo ulihusisha wasanii wengine kutoka sehemu mbalimbali duniani, akiwamo Angélique Kidjo kutoka Benin, Mohit Chauhan wa India, Sami Yusuf (Uingereza/ Azerbaijan), choirs pamoja na wanamuziki kutoka Marekani, Ulaya na Asia, wakishiriki kuimba “Vaishnav Jan To” kwa lugha na mitindo tofauti kama ishara ya umoja wa dunia katika kuenzi urithi wa Gandhi.  

Video ya wimbo huo ambao ulitayarishwa na Jowzeey mpaka kufikia sasa umetazamwa mara 298,291 katika mtandao wa YouTube.

Vanessa ambaye kwasasa anaishi Marekani na mpenzi wake Rotimi pamoja na watoto wao wawili, amewahi kutamba na ngoma mbalimbali ikiwamo Nobody But Me aliomshirikisha K.O, Niroge, Cash Madame, Hawajui, Kisela, Dume Suruali na nyinginezo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *