Hayo yamesemwa na Ikulu ya Ufaransa ya Elysee.

Viongozi hao wawili watajadili hatua zinazofuata katika mpango huo wa amani hasa katika maeneo ya usalama, utawala na ujenzi upya wa Gaza iliyoharibiwa vibaya na vita.

Mkutano huo pia unafuatia uamuzi wa Macron wa mnamo Septemba wa kutambua taifa la Palestina katika mkutano wa kilele wa Umoja wa Mataifa hatua ambayo Mamlaka ya Palestina iliisifu kama “ya kihistoria na ya ujasiri”.

Ni mwezi mmoja sasa tangu kufikiwa kwa makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano kati ya Hamas na Israel katika Ukanda wa Gaza, kufuatia miaka miwili ya vita iliyosababishwa na shambulio la Hamas la Oktoba 7, 2023 dhidi ya Israel.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *