#HABARI: Serikali imeanza kumkata shilingi milioni mbili kila siku mkandarasi anayejenga barabara za lami zenye urefu wa kilometa kumi na saba, zinazogharimu zaidi ya bilioni nane kwa Manispaa ya Geita mkoani Geita, baada ya mkandarasi huyo kushindwa kumaliza ujenzi wa barabara hizo kwa zaidi ya miaka miwili.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Bwana Martine Shigela ametembelea ujenzi wa barabara hiyo, na kuagiza kuchukuliwa hatua kwa mkandarasi huyo kwa kushindwa kumaliza ujenzi wa barabara hizo.
Mhandisi Mshauri wa mradi huo Mhandisi Richnold Manyanga anasema pamoja mkandarasi huyo kuongezwa miezi nane bado hajafikisha asilimia hamsini ya ujenzi wa barabara hizo kilometa kumi na saba.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.