#HABARI: Siku chache baada ya kuanza msimu wa mwaka 2025 wa upatikaji wa senene, katika maeneo ya Mkoa wa Kagera, baadhi ya wafanyabiashara wanaojihusisha na shughuli ya kuwatega na kuwauza, wameomba Serikali kupitia wataalamu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikamilishe utafiti unaofanywa wa kubuni, mitambo ya kuwatega na kuwanyonyoa kwa gharama nafuu.

Wafanyabiashara wa senene waliozungumza wakiwa kwenye eneo, lililoko karibu na daraja la Mto Kanoni linalofanyiwa matengenezo makubwa wamesema wanaingia gharama kubwa, kuwatega kwa kuwa wanatumia mitambo hafifu.

Wafanyabiashara wengine waliosema kuwa soko la senene kwa sasa sio kubwa kutokana na tatizo la upatikaji wa fedha, wameomba wakati wa msimu wa senene wawe wanapatiwa mikopo yenye riba nafuu ili waweze kupata mitaji ya kufanya shughuli hiyo.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *