Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliongezea mwaka mmoja mwengine mamlaka ya Kikosi cha Usalama cha Muda cha Umoja wa Mataifa kwa Abyei (UNISFA).

Azimio hilo lililowasilishwa na Marekani, lilipata kura 12 za ndio na tatu za Urusi, China na Pakistan zilijiepusha.

Naibu mjumbe wa Umoja wa Mataifa wa Marekani Dorothy Shea alikaribisha upya hatua hiyo na kusema, “Ingawa mamlaka hii inatofautiana na urekebishaji wa majukumu ya hapo awali, inalingana na lengo muhimu na la lazima la kuhakikisha kuwa ujumbe unaongozwa na vigezo vya wazi vinavyofuatilia maendeleo na kuhakikisha nchi mwenyeji zimewekezwa katika mafanikio ya ujumbe,” alisema.

Azimio lililoidhinishwa na Marekani lilibainisha kuwa Baraza hilo linapaswa “kuzingatia upyaji kuongezwa muda wa ujumbe huo kwa kuzingatia maendeleo yanayoonekana ya Sudan na Sudan Kusini.” Ilijumuisha vigezo vitatu, ambavyo wengi wa wajumbe wa Baraza hawakukubaliana lakini bado walipiga kura ya ndio kutokana na umuhimu wa uwepo wa UNISFA.

Chombo muhimu cha kuwajibisha serikali mwenyeji

Vigezo hivyo vinatoa wito wa kuondolewa kwa makundi yote yenye silaha ambayo hayajaidhinishwa kutoka Abyei, kuanzishwa tena kwa mikutano ya Mfumo wa Pamoja wa Kisiasa na Usalama (JPSM) kati ya Sudan na Sudan Kusini, na kuanzishwa kwa Polisi wa Usalama wa Pamoja wa Abyei.

“Vigezo hivi vitasaidia kuelezea athari za misheni na kutoa chombo muhimu cha kuwajibisha serikali mwenyeji kwa maendeleo yanayopimika,” mjumbe wa Marekani aliteta.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *