Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepiga kura Jumatatu, Novemba 17, kwa mpango wa amani wa Donald Trump huko Gaza, likiidhinisha haswa kupelekwa kwa jeshi la kimataifa, chini ya shinikizo kutoka Marekani ambalo ilionya juu ya hatari ya kuzuka tena vita. Ikiwa Mamlaka ya Palestina imeunga mkono azimio hilo, Hamas imelaani, ikisisitiza azimio ambalo “haikidhi mahitaji na haki za kisiasa na za kibinadamu” za Wapalestina.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Wajumbe wa kumi na tatu wa baraza hilo wamezungumza kwa niaba ya azimio hilo, ambalo balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Mike Waltz ameelezea kama la “kihistoria na lenye kujenga”. Urusi na China zimejizuia kupiga kura.

Azimio hilo la Marekani ambalo lilirekebishwa mara kadhaa wakati wa mazungumzo nyeti, “linasisitiza” mpango wa rais wa Marekani ambao uliwezesha kuanzishwa, mnamo Oktoba 10, makubaliano ya usitishaji mapigano kati ya Israel na Hamas katika eneo la Palestina lililoharibiwa na miaka miwili ya vita iliyosababishwa na shambulio la umwagaji damu la Hamas mnamo Oktoba 7, 2023.

Mpango wa kihistoria wa Rais Trump unaashiria mwanzo wa kile kitakachokuwa eneo lenye nguvu, thabiti, na mafanikio katika kufutilia mbali vurugu, chuki na ugaidi, amesea Mike Waltz, Balozi wa Marekani katik Umoja wa Mataifa.

Azimio hilo, ambalo shirika la habari la AFP, limeshuhudia, “linaidhinisha” uanzishwaji wa “Kikosi cha Kimataifa cha kusimamia amani” (ISF) kinachohusika haswa kwa kuunga mkono usalama wa mipaka kwa kushirikiana na Israel na Misri, kuhakikisha Gaza kutokuwa na silaha yoyote, kuwapokonya silaha makundi ya raia wanaozimiliki kinyume cha sheria, ulinzi wa raia na mafunzo ya jeshi la polisi la Palestina. Muundo wake haujatajwa.

Azimio hilo, linaloungwa mkono na Mamlaka ya Palestina, pia linaamuru hadi Desemba 31, 2027 “kamati ya amani”, taasisi ya “utawala wa mpito” huko Gaza hadi mageuzi ya Mamlaka ya Palestina. Kulingana na mpango wenye pointi 20 uliowekwa ndani yake, kamati hii itaongozwa na Donald Trump.

Kama rais wa Marekani amekaribisha haraka kupitishwa kwa mpango wake kwenye jukwaa lake la Truth Social – itafanya kuimarika kwa “amani zaidi ulimwenguni”, amesema -, hata hivyo, maswali mengi yanabaki juu ya mamlaka ambayo itasimamia ujenzi wa Gaza au kupokonya silaha makundi yenye silaha, kuanzia na Hamas. Matokeo? hali hi ambayo utekelezaji ngumu ambao bila shaka utafaidi Israel, aanaema Karim-Emile Bitar, profesa katika kitivo cha siasa huko Paris.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *