Japan imewasihi raia wake nchini China kuwa waangalifu huku kukiwa na mvutano unaoongezeka kati ya nchi hizo mbili kufuatia kauli za Waziri Mkuu wa Japan Sanae Takaichi kuhusu Taiwan, kisiwa kinachodaiwa na Beijing. 

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Mgogoro wa kidiplomasia ulmezuka baada ya Sanae Takaichi kusema mbele ya Bunge la Japan kwamba mashambulizi ya silaha kutoka China dhidi ya Taiwan yanaweza kuhalalisha kutuma wanajeshi wa Japan kulinda kisiwa hicho.

“Mnaposafiri, zingatieni semu mliko, hasa kwa uwepo wa watu wanaotiliwa shaka. Jaribuni kusafiri kwa vakundi inapowezekana,” inaonya taarifa iliyochapishwa Jumatatu kwenye tovuti ya Ubalozi wa Japan huko Beijing.

“Epukei maeneo yenye watu wengi au yale yanayoweza kutambuliwa kuwa yanatembelewa na raiawa Japan ” taarifa hiyo inaongeza.

Msemaji wa serikali ya Japani Minoru Kihara amesema leo Jumanne kwamba mapendekezo haya yalitolewa “kulingana na tathmini kamili ya hali ya kisiasa, ikiwa ni pamoja na hali ya usalama katika nchi au eneo husika, pamoja na hali ya kijamii.”

Mgogoro huo unatokana na matamshi yaliyotolewa na Waziri Mkuu mpya wa Japani, Sanae Takaichi, mnamo Novemba 7, ambapo alisema kwamba mashambulizi ya silaha dhidi ya Taiwan yanaweza kuhalalisha kutuma wanajeshi wa Japan kulinda kisiwa hicho chini ya vifungu vya “kujilinda kwa pamoja” vya sheria ya Japan iliyopitishwa mwaka wa 2015.

Taarifa hizi zilitafsiriwa kama ishara kwamba shambulio dhidi ya Taiwan—kisiwa ambacho uhuru wake unadaiwa na Beijing—linaweza kuhalalisha usaidizi wa kijeshi kutoka Tokyo hadi Taipei. Taiwan iko umbali wa kilomita 100 tu kutoka kisiwa jirani cha Japan.

Ubalozi wa China huko Tokyo uliona matamshi haya kuwa “ya uchochezi wa wazi,” ukibaini “yanaharibu sana hali ya mahusiano kati ya raia.”

Na katika ujumbe uliofutwa tangu wakati huo kwenye X, Balozi Mkuu wa China huko Osaka, Xue Jian, alitishia “kukata kichwa hicho kibaya bila kusita hata kidogo,” akimaanisha hotuba ya Bi. Takaichi.

Kujibu, Tokyo na Beijing ziliwarejesha nyumbani mabalozi wao wiki iliyopita.

Kutegemeana

Katika jaribio la kupunguza mvutano, Masaaki Kanai, afisa mkuu katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Japan kwa eneo la Asia-Pasifiki, aliwasili Beijing siku ya Jumatatu na kutembelea Wizara ya Mambo ya Nje ya China siku ya Jumanne, kulingana na shirika la habari la Jiji Press.

Anatazamiwa kukutana na mwenzake wa China, Liu Jinsong.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *