Jeshi la Sudan limetangaza siku ya Jumatatu, Novemba 17, kwamba limerejesha kwenye himaya yake mji wa Bara, ulioko Kordofan Kaskazini. Ulikuwa umedhibitiwa na Vikosi vya Msaad wa Haraka (RSF) tangu Oktoba 25. Mji wa Bara uliendelea kwa mara kadhaa kutekwa kutoka mikononi mwa upande mmoja kwenda upande mwingine.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kutekwa tena kwa mji wa Bara na jeshi la Sudan ni muhimu. Maendeleo haya katika mzozo yatakuwa muhimu kwa mustakabali wa mapigano huko El-Obeid, mji mkuu wa Kordofan Kaskazini, ambao bado unadhibitiwa na jeshi. Wanajeshi wa Sudan pia wanapiga hatua katika eneo hili, huku RSF wakiimarisha udhibiti wao katika mji wa Babanusa. Mapigano yanayoendelea kati ya wanajeshi wa RSF na wanajeshi wa Sudan yanaenea katika eneo lote la Kordofan.

Majimbo matatu yanayounda eneo hili yamekumbwa na vurugu, zaidi ya wiki mbili baada ya kuanguka kwa El-Fasher. RSF wanatafuta kupanua mashariki ili kuimarisha eneo lao, wakiwa tayari wamechukuwa udhibiti wa Darfur.

Jeshi na Vikosi vya Pamoja, ambavyo vilitangaza hali ya “tahadhari kwa ujumla” wiki iliyopita, vimeanzisha operesheni kubwa huko Kordofan Kaskazini. Tangu wakati huo wamechukua tena udhibiti wa baadhi ya maeneo, kama vile Kazkil, Um Dam Ahmed, na mji wa Um Syala, karibu na El-Obeid.

Siku ya Jumapili, Novemba 16, wanamgambo hao walianzisha mashambulizi yao makali zaidi dhidi ya Babanusa huko Kordofan Magharibi. Walipeleka idadi kubwa ya wapiganaji wao—kutoka El-Fasher—kuzunguka mji ambao tayari umezingirwa kabla ya kushambulia kambi ya Kikosi cha 22 cha jeshi. Katika kujibu, kikosi hiki kililenga maeneo ya RSF kuzunguka Babanusa, mji wa kimkakati ulioko kilomita 700 kutoka Khartoum, kwenye makutano ya njia za reli kati ya magharibi, mashariki na kaskazini mwa nchi, kwa kutumia ndege zisizo na rubani.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *