Katika kumbukumbu ya siku ya kuchapishwa ripoti ya “Mazingira ya Chuki”, Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kiislamu ya Uingereza (IHRC) imetangaza kuwa chuki dhidi ya Uislamu nchini humo haijapungua, bali pia imefikia hatua ya kutia wasiwasi zaidi katika mfumo wa kimuundo na kitaasisi; mwelekeo ambao una matokeo mabaya sana ya kijamii na kisiasa.

Katika ujumbe wake mpya wa video,IHRC imesoma tena ripoti yake ya miaka kumi iliyopita “Mazingira ya Chuki” (Environment of Hate), ikisisitiza kwamba chuki dhidi ya Uislamu nchini Uingereza imebadilika katika muongo mmoja uliopita kutoka tatizo la kijamii na kuwa mgogoro wa kimuundo.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, ongezeko kubwa la uhalifu wa chuki, ubaguzi uliopangwa, na kuakisiwa kibaguzi Waislamu katika vyombo vya habari ni matokeo ya ushirikiano wa taasisi tatu muhimu: siasa, sheria na vyombo vya habari, ambavyo vina nafasi ya moja kwa moja katika kuzalisha na kuendeleza mazingira haya ya uadui.

Ripoti ya awali ya Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kiislamu ya Uingereza (IHRC) ilionya kwamba takwimu rasmi kuhusu uhalifu unaofanywa dhidi ya Waislamu zinaficha picha halisi ya matukio hayo kutokana na kutoripotiwa ipasavyo. Tume hiyo inasisitiza kwamba pengo kati ya takwimu za serikali na hali halisi ya uwanjani limeongezeka, na hali hii inaondoa uwezekano wa kubuniwa sera nzuri.

Tume hiyo inaamini kwamba kushindwa kwa taasisi zinazowajibika kukabiliana na uhalifu wa chuki dhidi ya Waislamu kumefungua njia ya kuongezeka mfumo wa kibaguzi ambao ni zaidi ya chuki ya jadi kueneza propaganda chafu dhidi ya Uislamu na kuwa chuki na vita dhidi ya Uislamu.

Massoud Shajareh, Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Kibinadamu ya Kiislamu ya Uingereza, ameelezea hali hiyo kama kuvuka “mistari nyekundu” na kuonya kwamba uungaji mkono wa wazi wa baadhi ya wanasiasa na vyombo vya habari kwa mijadala potofu unazidisha hali hiyo kila mwaka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *