#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba linachunguza tukio la vifo vya pacha wawili wa kike wenye umri wa miaka 11 baada ya miili yao kupatikana wakiwa wananingʼinia kutoka katika kamba iliyofungwa juu ya mti.

Tukio la kujinyonga kwa watoto hao limetokea Novemba 17, 2025 majira ya saa 4.30 asubuhi katika Kijiji cha Kwale Mpona, Shehia ya Finya, Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Merehemu hao walikuwa ni wanafunzi wa darasa la tano katika Skuli ya Msingi Kizimbani Wete.

Tukio la kujinyonga kwa watoto hao liligunduliwa na Sada Mohammed Omar, ambaye ni mama mzazi wa watoto hao baada kuanza kuwatafuta na kufanikiwa kuona miili hiyo ikiwa inaning’inia juu ya mti umbali wa mita mia moja kutoka nyumbani kwao.

Miili ya marehemu hao imefanyiwa uchunguzi na daktari wa Hospitali ya Wilaya ya Wete iliyopo Kinyasini na kisha kukabidhiwa ndugu zao kwa ajili ya taratibu za mazishi ambapo uchunguzi wa awali unaonesha kuwa, sababu za tukio ni kukataa kufanya kazi za ndani walizoamrishwa na mama yao mzazi na kuamua kukimbilia nje na kwenda kusikojulikana ndipo miili yao ilipatikana wakiwa wameshajinyonga.

Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *