Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran amesema katika ujumbe wake kwamba: “Kuuliwa shahidi Sayyid na kinara wa mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu hakutasahaulika wala hakutasamehewa.”

Katika ujumbe wake uliotolewa kwa mnasaba wa tukio la Ashura na kumbukumbu ya kuuawa shahidi mjuu wa Mtume wetu Muhammad (SAW), Imam Hussein bin Ali (AS), Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Sayyid Abbas Araqchi ameandika: “Imam Hussein (amani ya Mwenyezi Mungu iwe juu yake) ndiye Bwana na Kinara wa Mashahidi, kwa sababu alisabilia kila kitu alichokuwa nacho (kwa ajili ya Mwenyezi Mungu) katika uwanda wa Karbala.”

Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran ameongeza kuwa: “Vivyo hivyo, hatutasahau wala kusamehe kuuliwa shahidi Ayatullah Sayyid Ali Khamenei, ambaye ni kiongozi na kamanda wa mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.”

Ujumbe huo wa Sayyid Abbas Araqchi umetolewa sambamba na maombolezo ya Muharram ambayo yalifikia kileleni nchini Iran jana tarehe 10 Muharram, siku inayojulikana kwa jila la Ashura ambapo mamiliomi ya watu walikumbuka mapambano ya Imam Hussein (AS) na watu wengine wa familia ya Mtume Muhammad (SAW) na wafuasi wao waaminifu waliuawa kikatili baada ya mapambano ya kishujaa yaliyobakia hai katika historia ya wanadamu.

Rais Pezeshkian: Ashura inahimiza kupambana na dhulma

Akizungumza adhuhuri ya Ashura katika Msikiti wa Imam Hussein huko Sahand, Mkoa wa Azarbaijan Mashariki, Rais Masoud Pezeshkian alisema, kuuawa shahidi Imam Hussein (AS) na damu safi ya mashahidi wa Karbala “vilianzisha mwendo wa historia unaoamsha akili zilizolala na kuwahimiza waliokandamizwa kupambana dhidi ya ukandamizaji.”

Rais Pezeshkian amesema maombolezo ya Imam Hussein (AS) yanapaswa kuonekane kwa vitendo, akisema ni kinyume na mantiki kumlilia Imam Hussein huku ukiendelea kufumbia macho dhulma, umaskini na njaa katika jamii.

“Njia ya Imam Hussein ni njia ya utu, heshima na mapambano dhidi ya ukandamizaji na dhulma, na hili lazima lionyeshwe kwa vitendo; maneno na kauli mbiu pekee hazitoshi,” amesisitiza Rais Pezeshkian.

Rais wa Jamhuri ya Kislamu amesema nchi iliyoongozwa na Imam Hussein (AS) inapaswa kuwa ya heshima na hadhi ambapo “hakuna Muirani wala mfuasi wa njia ya Imam Hussein anayepaswa kuteseka kutokana na umaskini, njaa au dhulma.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *