Nafuu ya usafiri mkoani Dar es Salaam inatarajiwa kurejea kuanzia Alhamisi, Novemba 20 mwaka huu, baada ya uongozi wa mkoa kutangaza kurejeshwa kwa huduma za mabasi ya mwendo wa haraka (BRT) katika njia ya Mbagala hadi katikati ya Jiji kama ilivyokuwa awali.
Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, aliyeelekeza UDART, DART, TANESCO na taasisi nyingine zilizo chini ya Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa kuhakikisha kuwa huduma hizo zinarejea rasmi katika njia ya Mbagala kuanzia tarehe hiyo, ili wananchi waendelee kupata usafiri wa uhakika na nafuu katika eneo hilo muhimu.
#AzamTVUpdates
✍ Esterbella Malisa
Mhariri| @claud_jm