
Zaidi ya mawaziri 80 wa maziringa wameungana kusisitiza haja ya dharura ya kuwepo mpango wa kimataifa wa kuachana na matumizi ya mafuka ya kisukuku, kauli wanayotoa baada ya hapo jana wanaharakati vijana kuwasilisha tamko lao kwenye kikao chao cha tatu cha mkutano wa COP30, ambapo walitaka nchi kuharakisha mchakato wa kuachana na matumizi ya mafuta hayo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Joseph Tsongo ni kijana ambaye siku ya Jumatatu katika mkutano wa COP30, alipewa tuzo kwa niaba ya Jambo Radio nchini DRC, kwa juhudi zao za kuelimisha jamii nchini Congo kujua haki zao linapokuja masuala ya mazingira
“Mazingira yako unayatunza kwa njia ipi, kwanza unaelezwa? Hiyo ndio kazi ambayo tunaifanya sisi kuwaelimisha hao watu.” Alisema Joseph Tsongo.
Mashiriki tofauti yasio ya kiserikali yameeleza haja ya kuwepo mchakato unaozingatia usawa na haki za jamii wakati nchi zikitafuta kuelekea uchumi wa kijani.
“Serikali za nchi ambazo ndizo zinaendelea sasa zikiwemo za Afrika zimesema kwamba kuja tu na nguzo hizi haitoshi. Lazima kuwekwe mikakati kabambe.” Alieleza Omar.
Tunapozungumzia mataifa kuachana na mafuta ya kisukuku, matumizi ya nishati safi kupikia inaweza kuwa na mchango katika jitihada za dunia kukabili mabadiliko ya tabianchi.
Profesa Askwar Hlonga anasema hili bado linahitaji jitihada zaidi.
“Mataifa mengi yametoa malengo yake ila kwa sasa asilimia kubwa za Afrika bado zipo kwenye matumizi ya asilimia 80 hadi 90 ya watu bado wanatumia nishati chafu.” Alieleza Profesa Askwar Hlonga.
Minzilet ijai, Belem, rfi Kiswahili.