Dar es Salaam. Vijana, tupunguze kusota kwa sababu ya ujinga wa pombe kupita kiasi. Mwisho wa mwaka huu, ni kile kipindi ambacho kila kijana anajiona kama “amefaulu maisha” hata kama akaunti iko kwenye mausoleum. 

Ni kipindi cha mavazi mapya, kelele za “Kesho hakuna kazi!” na stori za “Leo ni leo, kesho ni majaliwa.” Lakini pia ni kipindi ambacho walevi ni wengi kuliko waliopiga kura, na hospitali zinapokea vijana kuliko mitihani ya NECTA.

Sasa ngoja tuambiane ukweli. Kama wanaume kwa wanaume, wanawake kwa wanawake. Hata wale ambao hawataki kuji-identify kwa sasa. Ulevi kupindukia ndio chanzo cha drama nyingi kuliko mapenzi ya Gen Z.

1. Holiday Season sio Holiday Reason ya kuharibu maisha
Watu wengi wanaingia Desemba na roho ya “let me enjoy my money”, halafu wanaishia Januari na uso wa “Hata nauli ya daladala naomba niachie nishuke”. Lakini hatari zaidi ni kwamba uzembe unabadili likizo kuwa kitu kingine.

Holiday Season to Holiday Prison. Unadakwa kwa kosa la ‘kupushi’ ndinga ukiwa umelewa, au kupiga kelele usiku. Au kumtandika mtu ngumi. Holiday Season to Holiday ICU… ehh, ajali, ugomvi, madhara ya kupindukia.

Holiday Season to Holiday Kaburuni. Na hii ndio hatutaki kabisa kuisikia, maana hatuwezi ku-press next. Ndo tunasema, oya masela hebu jaribuni kuishi kwa akili basi. Enjoy yes. Lakini kujiua taratibu? Hapana tafadhali.

2. Pombe sio adui, lakini ulevi ndio kifo cha akili
Kunywa siyo kosa. Wale walevi walevu waliozoea kusoma “Drink Responsibly” kwenye chupa. Hao watakueleza, tatizo ni kwamba hakuna mlevi anayefanya hiyo responsibly. Ni kama kutafuta bikira wodi wa wazazi.

Mtu anakunywa hadi anasahau password ya simu. Anaanza kuongea lugha ya Roho Mtakatifu, halafu bado anataka kuendesha gari. Bro, wewe sio transformer na gari sio autobots. Itakutoa roho bila majadiliano.

3. Kuna vitu vinaweza kusubiri, lakini usalama wako hapana
Kupiga picha 37 na mwanga mkali wa kamera, inawezekana kusubiri. Kumfuata crush ambayo hata hajui jina lako, pia inaweza kusubiri. Dem kwenda kuongeza material kwa head, pia inaweza kusubiri. Kurudi home salama, hii haisubiri.

Desemba huwa kama mchezo wa kuigiza. Matamasha kila kona, sherehe kila weekend, bughudha nyingi. Lakini maisha yetu hayana “rewind button”. Ukiyachezea tu, hakuna editing. Ukija kushituka too late ushachelewa na mwana siyo wako.

4. Ulevi usiku, machozi asubuhi
Vijana wanasahau kitu kimoja: Pombe haina huruma. Leo hii unacheka, kesho yake unalia. Leo hii unainama kunywa, kesho yake unainama kwa maumivu. Leo hii unakimbiza “shots”, kesho yake unakimbizwa hospitali.

Tena usitufanye tuongee kuhusu zile stori za kuamka asubuhi bila simu, bila wallet, bila heshima. Na kabla hujatupa glass juu ukisema “cheers!”, jiulize, hivi kesho niache nini? Kilio ama kumbukumbu kuu na nzuri?

5. Vijana, tumieni akili hata kama mkilewa
Hata kama unatamani sana kuwa Superman wa pombe. Basi uwe Superman mwenye mpangilio:
Piga simu kwa suka ambaye ana taksii. Kabla hujazimika, wape rafiki simu yako. Usiondoke na watu usiowajua.

Ukiona kelele zimezidi, ondoka. Drama hutokea mara moja tu.
Na hii ndio punchline. Mwaka mpya hautaki kuanza ukivunjika mguu, ukibebwa stretcher, au ukiandika statement polisi ukiwa bado hujatulia kichwa.

6. Mwisho wa siku tunataka stori nzuri, sio rambirambi
Tunataka vijana waendelee kucheka, kuishi, kupiga kazi, kutafuta pesa, kupenda, kushindwa, kushinda. Siyo kuwa kwenye magazeti na headlines za huzuni. Desemba ni mwezi mzuri. Usiipe nafasi ya kukugharimu maisha.

Vijana, sherehe ni fire, lakini maisha ni moto zaidi. Chezeni lakini msichomeke. Ku-enjoy si vibaya, ila ku-overdo . Holiday Season iwe Holiday Reason ya kuishi, sio Holiday Prison, na sio Holiday Kaburuni.

Jilindeni bana!

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *