
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema kesho Jumanne, Desemba 2, 2025, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan atazungumza na wazee wa mkoa huo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu, ofisini kwake, Chalamila amesema mazungumzo hayo yataanza saa 5 asubuhi katika ukumbi wa mikutano ya Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
“Rais Samia atatumia fursa ya mkutano na wazee hao kulihutubia Taifa,” amesema Chalamila.
Amesema Rais Samia ataambatana na viongozi wa Serikali na wasio wa Serikali ambao watakuwa na mchango mkubwa kwenye mazungumzo hayo kwa mustakabali wa Taifa.
“NI mkutano mwafaka, unaorejesha matumaini na kuendelea kuponya pale ambapo Watanzania waliumia,” amesema Chalamila.