Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia askari magereza mwenye umri wa miaka 31 (jina limehifadhiwa kwa sababu za kiuchunguzi) kwa tuhuma za kumuua mke wake aliyetambulika kwa jina la Betia Oscar Chacha (25), mkazi wa Bugweto kwa kumkata na kitu kinachodhaniwa kuwa chenye ncha kali katika maeneo mbalimbali ya mwili na kumsababisha kifo.
Kamanda wa Polisi mkoani humo, SACP Janeth Magomi amesema mtuhumiwa amekamatwa na mwili wa marehemu umehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi wa kitabibu.
#AzamTVUpdates
✍ Kasisi Costa
Mhariri | @abuuyusuftz

(Feed generated with FetchRSS)