Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya iran amesema kuwa, manuva ya kupambana na ugaidi ya Sahand 2025 ni ishara ya nguvu ya mataifa huru dhidi ya madola ya kibeberu.

Spika Mohamed Qalibaf ameashiria manuva hayo yanayofanyika kwa ushirikiano na nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai na kusisitiza kuwa, mazoezi hayo yya pamoja yanadhihirisha irada na nguvu kubwa dhidi ya mataifa ya kibeberu.

Spika wa Bunge la Iran amebainisha kuwa, “Ushirikiano wa kiulinzi wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na hatua za pamoja za kukabiliana na ugaidi na nchi nyingine zinaendelea kuimarika, na matokeo yake ya kiutendaji yatadhihirika katika kuondosha uovu wa maadui wa Iran na kuyaangamiza makundi ya kigaidi.”

Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu ya Iran (Bunge la Iran)  ameongeza kuwa, kufanyika mazoezi haya ni ujumbe muhimu kwa madola ya kibeberu na kunaonyesha kuwa kuna dhamira kubwa miongoni mwa nchi huru za kujilinda dhidi ya uhusiano kandamizi wa kimataifa.

Mazoezi ya pamoja ya kupambana na ugaidi ya Sahand 2025, yaliyoandaliwa na kikosi cha ardhini la Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran SEPAH yameanza kufanyika leo katika Mkoa wa Azerbaijan Mashariki. Mazoezi hayo yanafanyika  kwa kushirikisha nchi tano wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Shanghai na yanahudhuriwa pia na  nchi waangalizi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *