Rais wa Colombia, Gustavo Petro, ameifananisha Israel na “utawala wa Nazi” katika maoni yake kuhusu vita vya kuangamiza vya Tel Aviv katika Ukanda wa Gaza.

Katika hotuba yake kwenye mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, Petro ameshambulia uvamizi wa Israel huko Gaza, akibainisha kuwa makumi ya maelfu ya watu wameuawa huko Palestina.

Ameeleza kwamba Waisraeli wamewanyeshea mvua ya makombora watu wa Palestina na hata watoto katika Ukanda wa Gaza, akisisitiza kwamba takwimu hizi haziwezi kufichwa, na hakuna maslahi ya kisiasa au kiuchumi yanayoweza kuficha ukweli huu.

Rais wa Colombia ameongeza: “Hiki ndicho kigezo halisi cha kile nitakachosema hapa, ambacho ni kwamba tumerudi kwenye enzi ya Wanazi.”

Mnamo Oktoba 7, 2023, Israel, ikisaidiwa na Marekani, ilianza vita vya zaidi ya miaka miwili vya mauaji ya kimbari huko Gaza, na kuua shahidi zaidi ya Wapalestina 73,000 na kujeruhi wengine 173,000, wengi wao wakiwa watoto na wanawake. Utawala huo ghasibu pia umesababisha uharibifu kwa 90% ya miundombinu ya eneo hilo.

Mnamo Mei 2024 Rais wa Colombia alitangaza kwamba nchi yake ingekata uhusiano wa kidiplomasia na Israel kwa sababu ina serikali na rais wanaofanya mauaji ya kimbari huko Gaza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *