Nigeria. Ndoa ya mwanamuziki nguli kutoka Nigeria, Innocent Idibia ‘2Baba’ imeanza kuchangamka hii ni baada ya kuzua gumzo katika mitandao ya kijamii kwa madai ya kuwa tukio lake la kukamatwa na polisi nchini Uingereza lilitokana na mkewe Natasha.

Tukio hilo lilidaiwa kutokea Oktoba mwaka huu, siku ambayo 2Baba alitarajiwa kufanya shoo nchini humo lakini mambo yalikwenda ndivyo sivyo ambapo baada ya kutua uwanja wa ndege alikamatwa na polisi na kushikiliwa kwa masaa kadhaa.

Kulingana na ripoti mbalimbali, zinaeleza kuwa Natasha aliamuru kukamatwa kwa mume wake huyo katika Uwanja wa Ndege muda mfupi baada ya 2Baba kuwasili. Vyanzo vinaeleza kuwa kukamatwa kwa msanii huyo kunatokana na mzozo mkubwa uliyotokea baina ya yeye na mkewe.

Hata hivyo tukio jingine linadaiwa kumkwaza Natasha ni kuwa alimwomba 2Baba amtambulishe kwa mashabiki wake, lakini inaelezwa kuwa msanii huyo alipuuzia ombi hilo jambo ambalo lilimfanya mwanamke ajisikie kutoheshimiwa. Wambea nchini Nigeria wanadai kuwa ndoa hiyo kwasasa inawaka moto japo wawili hao wanajitahidi kuficha mambo wakionesha kama wako sawa.

Aidha kufuatia na gumzo linaloendelea mitandaoni 2baba ameshare video kuwaomba radhi mashabiki kwa kukosa kuhudhuria kwenye show akida kuwa sababu kubwa alipata changamoto ya kiafya, huku akigoma kabisa kuelezea chanzo cha kukamatwa kwake.

“Kwanza kabisa, nawathamini wote mliojitokeza. Tulikuwa na dharura ya kiafya, ilikuwa ngumu, waandaaji na mashabiki wasiwe na wasiwasi, kwani tutaandaa upya na kufanya jambo jingine kubwa na zuri. Lakini pia tafadhalini sana kama hamjui jambo fulani, msianze kubuni mambo,”amesema 

Ikumbukwe 2Baba, alifunga ndoa ya kimila na mpenzi wake huyo anayedaiwa kuwa ni mjamzito Natasha Osawaru, sherehe ambayo ilifanyika Julai, 25,2025. Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa vyanzo vya karibu na familia, sherehe hiyo ya kitamaduni ilihudhuriwa na ndugu, jamaa wa karibu pamoja na wazazi wa 2Baba.

Msanii huyo aliyewahi kutamba na ngoma ya ‘African Queen’. Mwishoni mwa Januari 2025 alitangaza kutengana na aliyekuwa mke wake baada ya kudumu naye kwa miaka 13.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *