Siku ya Jumamosi, utawala huo wa kijeshi uliwateua watu 28 ikiwa ni pamoja na maafisa watano wa kijeshi kuongoza taifa hilo.

Mapema Waziri wa Mambo ya Nje wa Sierra Leone Timothy Kabba aliwaambia waandishi wa habari baada ya mikutano hiyo kwamba walikuwa na majadiliano yenye tija, huku pande zote zikielezea tofauti na wasiwasi wao.

“Leo tumekuwa na majadiliano yenye tija kubwa. Pande zote mbili zimeelezea wasiwasi wao. Kwa upande wa ECOWAS, mwenyekiti wa mamlaka alilaani mapinduzi hayo na ametoa wito wa kurejeshwa mara moja kwa utaratibu wa kikatiba, ambao ni pamoja na kuruhusu mchakato wa uchaguzi kumaliziwa.”

Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Guinea Bissau João Bernardo Vieira, kwa upande wake alisema baada ya majadiliano hayo:

Suluhisho la kurudi kwenye utaratibu wa kikatiba ni kuendelea kushirikiana na ECOWAS. Serikali ya mpito itadumu kwa mwaka mmoja, lakini suala hilo litawasilishwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa ECOWAS Disemba 14. Itategemeana na uamuzi wa sasa au utakaokuja, tutajua ni hatua zipi zitakazofuata.”

Nigeria | Wakuu wa nchi wa ECOWAS mjini Abuja 2023 | Ushirikiano wa kikanda
Rais wa Guinea-Bissau aliyepinduliwa Umaro Sissoco Embaló akiwa kwenye kikao 64 cha kawaida cha Wakuu wa Nchi na Serikali cha Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) huko Abuja mnamo Desemba 10, 2023.Picha: Kola Sulaimon/AFP

Mapinduzi yaiengua Bissau kwenye maamuzi, ECOWAS

Kufuatia mapinduzi hayo, mataifa wanachama wa ECOWAS waliisimamisha Guinea Bissau kwenye vyombo vyake vyote vya kutoa maamuzi.

Rais Umaro Sissoco Embalo amekimbilia Jamhuri ya Kongo, hii ikiwa ni kulingana na vyanzo kadhaa, na tayari serikali hiyo ya kijeshi imemteua Jenerali Horta N’Tam kuwa mkuu wa utawala wa mpito ambao unatarajiwa kuwepo kwa mwaka mmoja. Mamlaka hiyo imetetea mapinduzi hayo ukisema unataka kuushughulikia mtandao wa dawa za kulevya unaosababisha machafuko nchini Guinea-Bissau.

Maamuzi zaidi ya jumuiya hiyo yanatarajiwa kuchukuliwa kwenye mkutano wa kilele wa Disemba 14, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa vikwazo.

Senegal na Guinnea Bissau zinazopakana zimepitia kwenye mapinduzi ya mara nne na ya majaribio ya mara nne tangu uhuru kutoka Ureno mwaka 1974. Guinea Bissau inaungana sasa na Burkina Faso, Mali, Madagascar, Niger na Sudan kwenye orodha ya mataifa yaliyosimamishwa uanachama wa Umoja wa Afrika kufuatia mapinduzi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *