Tume ya Vyuo Vikuu Nchini (TCU) imesitisha kibali cha udahili na usajili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Mwanza kutokana na ukiukaji wa sheria, pamoja na udahili wa idadi kubwa ya wanafunzi kuliko uwezo wa chuo hicho.

Taarifa hiyo imetolewa leo na Katibu Mtendaji wa tume hiyo, Prof.Charles Kihampa ambapo amewahakikishia wanafunzi waliodahiliwa kupata vyuo vingine wakati wakisubiri tume itakayoundwa kuchunguza na kuchukua hatua dhidi ya chuo hicho.

#AzamTVUpdates
✍ Innocent Aloyce
Mhariri | @claud_jm

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *