#HABARI: Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu Dkt. Dorothy Gwajima, ametoa ahadi ya kuendeleza ushirikiano na Mabaraza ya Wazee nchini.

Amesema lengo la hatua hiyo ni kuongeza utoaji wa elimu na kuwaweka wazee karibu na vijana ili kujenga vizazi vyenye maadili, uzalendo na umoja wa kitaifa.

Dkt. Gwajima amesema kuwa kwa kushirikiana na wizara za kisekta na wadau wote stahiki, wizara yake itatekeleza maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia mabaraza ya ngazi zote, ambayo ni takribani 20,768.

Aidha, amesema kuwa wazee wataendelea kushirikishwa kikamilifu katika mijadala na shughuli za kijamii, wakihimiza amani na uzalendo miongoni mwa vijana, kwa mustakabali chanya wa Taifa.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *