Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu, Amnesty limetoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi huru kuhusu mashambulio yaliyofanywa na wapiganaji wa RSF kwenye moja ya kambi kubwa ya wakimbizi huko kaskazini mwa jimbo la Darfur, mwanzoni mwa mwaka huu.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Katika ripoti yake Amnesty International imesema Mwezi wa Aprili mwaka huu RSF ilivamia kambi ya Zamzam  na kuuteka mji wa el-Fasher na ikitekeleza ukatili wa kibinadamu ikiwa ni pamoja na kunyonga raia,ubakaji,unyanyasaji wa kijinsia, na uharibifu wa shule, misikiti pamoja na hospitali.

Ripoti  hiyo ya Amnesty ni mojawapo ya ripoti za hivi punde za mashirika ya kutetea haki za binadamu kuishtumu RSF kwa vitendo vya ukatili katika vita vya  takariban miezi 30 vya Sudan, hasa eneo la Darfur wakati huu pia  Jeshi la Sudan vile vile  likishutumiwa kwa ukatili huohuo.

Makabiliano kati ya RSF na jeshi la Sudan yalizuka  mwezi Aprili 2023, Mgogoro huu ukisababisha vifo vya watu karibia laki 4  na kuwaacha wengine millioni 14 bila makao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *