
Hayo yameelezwa Alhamisi na msemaji wa serikali, Vincent Magwenya akisema kwamba Afrika Kusini haitoshiriki mikutano kadhaa ya G20 ya mwaka 2026 na itarejea tena wakati urais wa G20 utakapokabidhiwa kwa Uingereza mwaka 2027.
Magwenya ameandika katika mtandao wa kijamii kwamba kwa sasa watapumzika kwa muda hadi watakaporejea tena katika programu za kawaida.
Marekani yachukua urais wa mwaka mmoja
Amesema Afrika Kusini haikutarajia nchi nyingine za G20 kuususia urais wa Marekani au kushawishi ijumuishwe.
Mwezi huu, Marekani imechukua urais wa mwaka mmoja wa G20, baada ya kususia kwa kiasi kikubwa mikutano ya Afrika Kusini, ukiwemo ule wa kilele uliofanyika mwezi Novemba mjini Pretoria.