Mwakilishi wa Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Seyyed Ali Khamenei katika Baraza la Ulinzi la Iran amelionya Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba ya Uajemi dhidi ya madai “yasiyo ya kujenga” kuhusu visiwa vitatu vya Iran na visima vya gesi vya Arash.

Ali Shamkhani alitoa onyo hilo kupitia ujumbe katika akaunti yake ya X siku ya Alhamisi, akiashiria tamko la mwisho la Mkutano wa 46 wa Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba ya Uajemi uliofanyika Bahrain Jumatano.Katika tamko lake, baraza hilo liliendeleza msimamo wake wa muda mrefu kuhusu visiwa vya Tunb Kubwa, Tunb Ndogo, na Abu Musa vilivyoko Ghuba ya Uajemi, likisisitiza tena kuunga mkono madai ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) juu ya mamlaka ya visiwa hivyo.

Baraza limedai kuwa visiwa hivyo ni sehemu ya ardhi ya UAE.

Tamko hilo pia lilidai kuwa umiliki wote wa visima vya gesi vya Arash uko ndani ya maji ya Kuwait, na kwamba rasilimali zake zote ziko pekee katika eneo la pamoja la Kuwait na Saudi Arabia.

Katika ujumbe wake, Shamkhani alieleza masuala hayo kuwa ni “mistari myekundu” ya Iran. Amesema: “Wajibu wa majirani ni kuunda usalama, si kucheza na mistari myekundu ya taifa la Iran.”Alionya kuwa madai ya Baraza la Ushirikiano la Nchi za Ghuba ya Uajemi kuhusu visiwa vya Iran na visima vya gesi vya Arash yameibuliwa tena katikati ya vitendo vya uharibifu vya Marekani na utawala wa Kizayuni.

Admeri Shamkhani ambaye aliwahi kuwa waziri wa ulinzi wa Iran, amesisitiza kuwa Iran ilijizuia wakati wa vita vya siku 12 vya kichokozi vya Marekani na utawala wa Kizayuni wa Israel katikati ya Juni licha ya baadhi ya nchi kuunga mkono uvamizi huo, akionya kuwa “nguvu ya Iran katika Ghuba ya Uajemi haipaswi kutafsiriwa vibaya.”Visiwa vya Ghuba ya Uajemi vya Abu Musa na Tunb Kubwa na Ndogo kihistoria ni mali ya Iran, jambo lililothibitishwa na rekodi nyingi za kihistoria, kisheria, na kijiografia ndani ya Iran na kimataifa. Hata hivyo, UAE imekuwa ikidai mara kwa mara visiwa hivyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *