#HABARI: Katibu wa Siasa na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dodoma, Jawadu Mohamed, ameipongeza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema imeonesha msimamo thabiti wa kutetea maslahi ya Taifa na kukemea vikali jitihada zozote za mataifa ya nje kuingilia mambo ya ndani ya Tanzania.
Amesema hotuba hiyo, ambayo imeandaliwa kwa kuzingatia uchunguzi na utafiti wa kina, ni miongoni mwa hotuba bora zaidi zilizowahi kuimarisha umoja wa kitaifa tangu tukio la machafuko ya Oktoba 29, katika kipindi cha uchaguzi mkuu nchini.
Jawadu ameongeza kuwa pamoja na kuwepo kwa wachache wanaoikosoa au kutoikubali hotuba hiyo, idadi yao ni ndogo sana na kwamba Mataifa ya Afrika yaliyojikuta yakikumbwa na migogoro kutokana na kuruhusu kuingiliwa kwa masuala yao ya ndani, akitaja Sudan, Somalia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na mengineyo.
Kwa mujibu wake, hotuba ya Rais Samia ni tahadhari ya busara kwa Tanzania ili kuendeleza amani, utulivu na umoja wa kitaifa, na kuepusha nchi kuangukia kwenye misukosuko kama ile inayozikumba baadhi ya nchi katika bara la Afrika.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.