Kundi la kutetea wafungwa wa Kipalestina, The Palestinian Prisoners’ Society (PPS), limeonya juu ya njama hatari ndani ya magareza ya Israel ya kumuua kiongozi mtajika wa Palestina, Marwan Barghouthi, aliyetekwa nyara huku kukiwa na ripoti za ukandamizaji na kudhalilishwa pakubwa kiongozi huyo wa Palestina.

Israel inafanya njama ya kumuuwa Marwan Barghouthi huku mashinikizo ya kimataifa yakiongezeka ili kuaachiwa huru kiongozi huyo wa Palestina. 

Kundi hilo la kutetea wafungwa wa Kipalestina  limetangaza kuwa kushtadi mashambulizi dhidi ya Barghouthi kunadhihirisha malengo ya kutisha ndani ya utawala ghasibu wa Aviv ili kummaliza kiongozi huyo mtajika wa Palestina.

Amjad al Najjar Mkurugenzi wa The Palestinian Prisoners Society (PPS) ameuomba Umoja wa Mataifa na taasisi za kimataifa kuingilia kati bila kuchelewa. 

Aidha ametoa wito kwa kamati ya Umoja wa Mataifa kumtembelea Barghouthi, kutathmini hali yake akiwa kizuizini na kuushinikiza utawala wa Israel ili umwachia huru na kushughulikia hali yake ya kiafya kabla hali haijakuwa mbaya zaidi. 

Ripoti zinasema kuwa Barghouthi ana hali mbaya baada ya familia yakekusema kuwa imearifiwa kuhusu unyanyasaji na ukatili anaokumbana nao katika magereza ya Israel. 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *