
Merz amedokeza kuwa mchakato wa amani huko Gaza utakuwa mojawapo ya masuala ya kipaombele katika ajenda ya mkutano wake na Netanyahu.
Changamoto za mahusiano baina ya nchi hizo mbili pia zitajadiliwa, baada ya Merz kuweka kizuizi kwa baadhi ya silaha zinazouziwa Israel katika kukabiliana na operesheni inayofanywa na jeshi la Israel katika Ukanda wa Gaza .
Merz pia anatazamiwa kuangazia suala linalokithiri la chuki dhidi ya Wayahudi nchini Ujerumani.
Hivi karibuni, balozi wa Israel nchini Ujerumani, Ron Prosor, alionya juu ya chuki ya mrengo wa kushoto kwa Wayahudi.