Wakati wa mkutano wa kila wiki na waandishi wa habari, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Iran Esmail Baghaei amesema katika siku zijazo, karibu raia 50 hadi 55 wa Iran watarejea nchini humo.

Baghaei amesema hilo ni kundi la pili katika miezi ya hivi karibuni kurejea Iran.

Msemaji huyo amekosoa kile alichokiita “vitendo vya kibaguzi vya Marekani dhidi ya raia wa kigeni, hasa raia wa eneo lao na hasa Wairani”.

Ameongeza kuwa ni dhahiri kwamba shinikizo hizo zimechochewa kisiasa na kwamba sera hizo za kupinga uhamiaji zinakinzana na sheria za haki za binadamu.

Kwa mujibu wa CNN, kundi hilo linatarajiwa kuwasili Iran baadaye leo baada ya ndege wanayosafiria kusimamia kwa muda nchini Kuwait.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *