Wanafunzi hao wamewasili mjini Abuja na kukabidhiwa kwa viongozi tawala. Hayo yameelezwa siku ya Jumapili na chanzo kimoja cha Umoja wa Mataifa bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi ikiwa mpango huo ulifikiwa kupitia mazungumzo au nguvu za kijeshi, huku hatima ya wanafunzi wengine 165 na wafanyakazi kadhaa waliotekwa ikiwa bado haijulikani.

Mwishoni mwa mwezi Novemba, wanafunzi 315 na wafanyakazi walitekwa nyara kutoka shule ya bweni ya Mtakatifu Maria iliyoko kaskazini mwa jimbo la Niger. Takriban wanafunzi 50 walitoroka muda mfupi baadaye. Makundi yenye silaha nchini  Nigeria  yamekuwa yakiwateka watu na kudai kikomboleo, kama njia ya kujipatia fedha kwa haraka.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *