
Katika tamko lake lililotolewa Disemba 7, Mufti Zubeir alisema mazungumzo hayo yanaendeshwa kwa usimamizi wa Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Nuhu Mruma.
“Mazungumzo yameanza kupitia Taasisi ya Tanzania Interfaith Partnership (TIP), ambayo kwa sasa inasogezwa na Katibu Mkuu wa BAKWATA, baada ya Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) kumaliza kipindi chake cha usimamizi,” alisema Mufti Zubeir.
Alisisitiza kuwa viongozi wa dini wana jukumu la kuendeleza amani na heshima ndani ya jamii, na kuwa “tusiruhusu dini au imani ziwe njia ya kuwahamasisha watu kufanya maandamano yanayoweza kuleta mgogoro”.