Dar es Salaam. Pata picha mtoko wa Prof. Jay na Chemsha Bongo. Sogea naye hadi Bongo Dar es Salaam, kisha Piga Makofi na Ndiyo Mzee. Hadi hapo Promota Anabeep mpigie ili kwake liwe Zali la Mentali. Weka kando Jina Langu. 

Hizi ngoma hazina vichupa hata zenye vichupa siyo vikali. Yaani audio kali kuliko ‘kwalite’ ya kideo chake. Hii ilifanya wanyamwezi wengi wapotezee kufanya video, na kuacha mipini katika mwendo wa audio pekee. ‘Iliwakosti’ sana.

Ngoma zinatunzika vizuri kwenye kideo kuliko audio pekee. Fumba macho pata picha mkono kama Bongo Dar es Salaam. Ukutane na wahuni wa leo waliweke kwa chupa? Yaani mishe za Daslama zote kideoni. Dude akasome. 
Kasikilize Binti ya LadyJadee, ni vipi ingepewa haki ya kuishi kwa kideo kikali cha dunia ya leo? Vipi Kamanda ya Daz Nundaz? Barua je? Kama Unataka Dem Jaymoe? Vipi dude la dunia Mtoto wa Geti Kali ya Inspekta Haroun Babu?

Kuna Nje Ndani ya Gangwe Mob na Hili Game ya Nature. Ni wazi kwamba zamani chakula kitamu kilipikwa na kuwekwa kwenye vyombo chakavu. Mashairi na midondoko ilikuwa ya dunia ya sasa, sayansi ya video ilizingua.
Leo hii vichupa vitamu kinyama. Lakini mashairi na mitambao ni maseke matupu. Yaani mapini ya kawaida mavideo makali, zamani pini kali mavideo ya kibwege. Ni kwamba wale wangezaliwa leo na wa leo wangezaliwa zamani.

Achana na wale wa kuimba, hapa naongelea michano. Masela wa kubum kabam wanaiga swaga za jeje, wakati zamani jeje waliiga swaga za kubum kabam. Jaribu kuwaza “Hawatuwezi” lingetoka leo. Kuna pini la kubato nalo?

Prof. Jay alikosa video kali, huyu Lunya anakosa mashairi makali. Ndo tofauti ilipo. ‘Ofu kozi’ hata mibiti mitamu hadi unyamwezini uzalishaji wake wa kiwaki. Siyo kwamba naroa shavu kqa zile za kitambo. Ni ukweli ndo uko hapo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *