Kikundi cha Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu DRC kimetoa ripoti yake ya hivi punde kuhusu mgogoro mashariki mwa nchi, ingawa, rasmi, kila upande umeahidi kusitisha mapigano, iwe Washington au Doha. Lakini, kulingana na Umoja wa Mataifa, licha ya maendeleo ya kidiplomasia, hali ya usalama inaendelea kuzorota, huku mapigano yakizidi kuwa makali.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Ripoti hii inaweza kusababisha ghasia huko Kinshasa, Goma… na Kigali.

Kikundi cha Wataalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu DRC kimewasilisha ripoti yake ya katikati ya muhula, hati ambayo RFI iliweza kupata kabla ya kuchapishwa.

Wataalamu wanawaelekeza maafisa wa jeshi la Kongo wanaoshutumiwa kudumisha uhusiano na waasi wa Kihutu wa Rwanda (FDLR), kundi linalochukuliwa na Kigali kuwa lilihusika katika mauaji ya kimbari, na Kigali yenyewe, inashutumiwa si tu kwa kuunga mkono AFC/M23 bali pia kwa kupeleka wanajeshi wake katika ardhi ya Kongo na kufanya ukatili katika maeneo mbalimbli.

Kati ya wanajeshi 6,000 na 7,000 wa Rwanda bado wako mikoa ya Kivu 

Kulingana na wataalamu wa Umoja wa Mataifa, baadhi ya wanajeshi wa Rwanda wapo hata ndani ya kikosi cha polisi cha AFC/M23.

Tangu mwezi Aprili 2025, vitengo vya Jeshi la Ulinzi la Rwanda (RDF) vimefanya operesheni za pamoja na AFC/M23 katika jaribio la kuwaangamiza FDLR. Hatua hizi, zilizoandikwa na wataalamu wa Umoja wa Mataifa, zimeshindwa, kulingana na ripoti hiyo, kuwalenga viongozi wa FDLR katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Hati hiyo pia inaelezea upanuzi wa uwepo wa AFC/M23-RDF katika mkoa mwingine, Kivu Kusini, kupitia mihimili kadhaa kati ya Walungu, Mwenga, Uvira, na Kalehe, kwa usaidizi wa Twirwaneho, kundi lingine lenyr uhusiano na AFC/M23.

Wataalamu wanakadiria kuwa kati ya wanajeshi 6,000 na 7,000 wa Rwanda bado wamepelekwa katika mikoa miwili ya Kivu. Kigali na AFC/M23 zinakanusha madai haya

Ushirikiano wa kudumu na FDLR

Kwa upande wake, Kinshasa inaendelea kuyategemea makundi yenye silaha yanayojitolea kwa Ulinzi wa Nchi (VDP), VDP/Wazalendo, kama kikosi kinachoshirikiana na jeshi la FARDC kudhibiti AFC/M23 na wanajeshi wa Rwanda.

Ripoti pia inaangazia ushirikiano unaoendelea na FDLR, licha ya ahadi rasmi za kuangamiza kundi hili.

Tangu mwezi Juni 2025, VDP/Wazalendo na FDLR wamekuwa wakiendesha mashambuliziya kuvizia dhidi ya AFC/M23 na RDF, ili kuchukua ngome zao au kuvuruga njia zao za kusafirisha chakula na vifaa vya kijeshi.

Ufunuo mwingine kutoka kwa ripoti hii: wakati FARDC ilipowataka rasmi FDLR kusalimisha silaha zao mwezi Oktoba, tangazo hili lilileta mvutano. Kulingana na wataalamu, baadhi ya maafisa wa Kongo walijaribu kuwahakikishia FDLR kuhusu mwendelezo wa ushirikiano wao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *