Rais Alassane Ouattara ameapishwa leo Jumatatu Desemba 8, 2025, kwa muhula wa nne kama raia wa Côte d’Ivoire, wakati wa sherehe katika ikulu ya rais huko Abidjan. Alichaguliwa tena mwishoni mwa mwezi Oktoba kwa karibu 90% ya kura katika duru ya kwanza.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Abidjan, Bineta Diagne

Akiwa ameweka mkono wake wa kushoto kwenye Katiba na mkono wake wa kulia akiuinua, Alassane Ouattara ameapishwa. Rais wa Baraza la Katiba, Chantal Nanaba Camara, kisha akazungumza ili kuthibitisha rasmi kuchukuwa kwake rasmi mamlaka.

Kisha akahutubia hadhira teule. Amewashukuru wakuu kumi na wawili wa nchi waliosafiri kuhudhuria sherehe hiyo. Miongoni mwao ni Denis Sassou-Nguesso wa Kongo, Brice Oligui Nguema wa Gabon, pamoja na marais wa zamani kama vile Mahamadou Issoufou wa Niger na Nana Akufo-Addo wa Ghana.

Yaël Braun-Pivet, Rais wa Bunge la Ufaransa, amemwakilisha rais Emmanuel Macron.

Mamlaka ya “mabadiliko ya vizazi”

Alassane Ouattara amewashukuru raia wa Côte d’Ivoire. “Uchaguzi huu unaonyesha chaguo la utulivu,” amesema. “Uchaguzi huu unaonyesha uelewa wa masuala katika eneo dogo, ambapo changamoto ni ngumu,” ameongeza.

Alassane Ouattara ameahidi kwamba mamlaka hii itakuwa ya “mabadiliko ya vizazi”: “Ni kitendo cha uwajibikaji na ukomavu wa kisiasa,” amebainisha.

Alassane Ouattara anataka kuona kuibuka kwa “wasomi waaminifu, wenye uwezo wa kisiasa na kiutawala waliojitolea kwa dhati kwa maslahi ya umma.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *