Kitendo hiki cha ukatili kimebeba uzito mkubwa wa kisiasa katika sehemu hii ya mji mtakatifu, unaokaliwa na Israel tangu 1967, ambako shirika la Umoja wa Mataifa la Msaada kwa Wakimbizi wa Kipalestina UNRWA, sasa linachukuliwa kama lisilotakiwa tena ( Persona-non-grata).

Kwa mujibu wa Philippe Lazzarini, Kamishina Mkuu wa UNRWA, “maafisa wa usalama wa Israeli, wakiwa wameambatana na maafisa wa manispaa, waliingia kwa nguvu kwenye majengo ya shirika hilo, ambako walikata mawasiliano yote, kuchukua samani na vifaa vya kompyuta, na kubadilisha bendera ya bluu ya Umoja wa Mataifa kwa bendera ya Israeli.”

Kupitiamtandao wake wa kijamii wa  Lazzarini alilaani vikali akisema “Kitendo hiki kipya kinaonesha dharau ya wazi kwa wajibu wa Israel kama nchi mwanachama wa Umoja wa Mataifa, wa kulinda na kuheshimu kutoharibiwa kwa majengo ya Umoja wa Mataifa”.

Vita huko Gaza vimesababisha idadi kubwa ya mashambulizi dhidi ya majengo na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

Vita huko Gaza vimesababisha idadi kubwa ya mashambulizi dhidi ya majengo na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa.

Miezi ya kunyanyaswa

Kabla ya hatua hii ya mamlaka za Israeli, UNRWA imeshuhudia kuongezeka kwa shinikizo baada ya “miezi ya unyanyasaji iliyojulikana kwa maandamano ya uhasama, matukio ya moto mwaka 2024, kampeni ya upotoshaji dhidi ya shirika hilo na vitisho vya mara kwa mara.”

Muhimu zaidi, amesema UNRWA inalengwa na sheria mbili zilizopitishwa na Knesset mwezi Oktoba. moja ikipiga marufuku shughuli za shirika hilo kote Israel, ikiwemo Jerusalem Mashariki, na nyingine ikimzuia afisa yeyote wa Israeli kushirikiana na wafanyakazi wake.

Chini ya shinikizo hili linaloongezeka, shirika lililazimika mwishoni mwa Januari kuhamisha makao yake makuu katika kitongoji cha Sheikh Jarrah na kupeleka kwa muda wafanyakazi wake wa kimataifa nchini Jordan.

Jinsi ilivyokuwa ofisi ya UNRWA Gaza

Ziad Taleb

Jinsi ilivyokuwa ofisi ya UNRWA Gaza

Ukiukaji wa kutoharibu majengo ya UNRWA

Lakini Lazzarini amesisitiza kuwa “hakuna sheria ya kitaifa inayoweza kufuta hadhi ya kimataifa ya makao makuu ya UNRWA. UNRWA inabakia kuwa kituo cha Umoja wa Mataifa, na hivyo inalindwa dhidi ya aina yoyote ya kuingiliwa,” amesema Lazzarini,

Israel ni mshiriki wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa kuhusu Kinga na Misamaha, ambao unatoa hadhi ya “kutoshambuliwa kwa majengo ya Umoja wa Mataifa, yakilindwa dhidi ya upekuzi, ukamataji na kulinda mali zake dhidi ya hatua yoyote ya kisheria.

Mahakama ya Kimataifa ya Haki yenyewe imesisitiza kuwa Israel ina wajibu wa kushirikiana na UNRWA.

“Hakuna ubaguzi wowote unaoweza kukubalika,” amesisitiza mkuu wa shirika hilo. “Kukiuka hili kutaunda mfano hatari popote pale Umoja wa Mataifa ulipo.”

Ingawa wafanyakazi wa kimataifa wa UNRWA walilazimika kuondoka mjini, wafanyakazi wake wa ndani wanaendelea na kazi yao, mara nyingine wakiweka maisha yao hatarini, kuwasaidia Wapalestina walioathirika vibaya na mgogoro wa kibinadamu katika Ukingo wa Magharibi na vita huko Gaza.

Kamishina Mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini

Kamishina Mkuu wa UNRWA Philippe Lazzarini

Msaada mpya kwa shirika hilo

Uvamizi huo wa leo Jumatatu unakuja siku tatu tu baada ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhuisha mamlaka ya UNRWA kwa miaka mingine mitatu. Uamuzi huo ulifikiwa kupitia kura ya wengi kwa kishindo, jambo ambalo Lazzarini amelisifu kama ishara ya mshikamano wa kimataifa usiotetereka.

“Hii inaonesha mshikamano mkubwa duniani kote kwa wakimbizi wa Kipalestina,” amesema Lazzarini, akiongeza kuwa kuhuishwa huku pia kunamaanisha kutambuliwa kwa wajibu wa jumuiya ya kimataifa kwa watu waliotawanywa, wahanga wa kile ambacho kimeelezwa kuwa ukaliaji haramu kwa miaka 75.

Lakini si hilo tu: “Kura hii sasa lazima itafsiriwe kuwa dhamira halisi na rasilimali za kutosha ili kutekeleza kikamilifu mamlaka,” ameongeza.

Kati ya ukatili wa uvamizi wa polisi na uzito wa kuhuishwa kwa mamlaka ya Umoja wa Mataifa, UNRWA tena inajikuta katikati ya mapambano ya kisiasa ambayo yanazidi kuathiri sana opereshen zake za kibinadamu.

Shule zake, kliniki na huduma za kijamii, ambazo ni muhimu kwa mamilioni ya wakimbizi wa Kipalestina Mashariki ya Kati, zimekuwa kitovu cha mvutano ambapo sheria za kimataifa zinakutana uso kwa uso na ukaliaji wa Israeli katika ardhi ya Palestina.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *