Leo ikiwa ni siku ya 40 tangu 29 Oktoba, ambapo Tanzania ilifanya Uchaguzi Mkuu, ambapo baadae ulikumbwa na vurugu zilizosababisha mauaji ya wananchi ambao mpaka leo idadi kamili haifahamiki.
Licha ya polisi kulaumiwa kwa kutumia nguvu iliyopitiliza, Rais Samia, amewatetea polisi kwa kusema kuwa vikosi vya usalama vililazimika kutumia “nguvu muafaka” kukabiliana na waandamanaji aliowataja kuwa hawakuwa na nia ya amani.
Wakati hayo yakiendelea, mataifa kadhaa ya Magharibi yametoa wito kwa Tanzania kuheshimu haki za binadamu na kulinda uhuru wa kujieleza.
Pamoja na mvutano uliopo, Rais Samia ametangaza wito wa maridhiano yasiyokuwa na masharti.
Hata hivyo, bado haijafahamika wazi iwapo upinzani utakubali kuketi meza moja na serikali, na kama wakikubali, mazungumzo hayo yatafanyika chini ya mazingira gani.