
Zelensky alikutana kwanza na viongozi wa Uingereza, Ufaransa na Ujerumani jijini London kabla ya kuelekea Brussels baadaye jana kwa mazungumzo na wakuu wa Umoja wa Ulaya na NATO.
Na kwenye mkutano na waandishi wa habari, alisema suala la maeneo bado linasalia kama moja ya mambo muhimu yaliyokwama katika mazungumzo.
“Je, tunafikiria kusalimisha eneo lolote? Hatuna haki ya kisheria ya kufanya hivyo. Kulingana na sheria ya Ukraine, katiba yetu, na sheria ya kimataifa, hatuna haki ya kimaadili ya kufanya hivyo pia. Urusi inasisitiza tuwape eneo, lakini hakika hatutaki kutoa chochote,” alisema Zelensky.
Baadaye, Zelensky alisema kupitia mtandao wa X kwamba alikuwa na “mkutano mzuri na wenye tija” na mkuu wa NATO Mark Rutte, Rais wa Baraza la Ulaya Antonio Costa na Rais wa Tume ya Ulaya Ursula von der Leyen.