
Vyombo vya habari vya Israel vimeripoti kwamba Netanyahu atakwenda Marekani kati ya Disemba 28 hadi Januari 4, ingawa msemaji wa serikali amekataa kuthibitisha taarifa hizo.
Kituo cha utangazaji cha cha N12 kimeripoti kwamba Netanyahu atakutana na Trump mara mbili na atafikia kwenye makazi ya Trump yaliyoko Mar-a-Lago, Florida.
Huku hayo yakiendelea jeshi la anga la Israel limeshambulia tena maeneo ya wanamgambo wa Hezbollah wanaoungwa mkono na Iran kusini mwa Lebanon, hii ikiwa ni kulingana na jeshi hilo mapema leo.