#HABARi: Jeshi la Polisi limetoa taarifa kuwa, hadi muda huu wa mchana Desemba 9, 2025 hali ya usalama wa nchi ni shwari.
Vyombo vya ulinzi na usalama vinaendelea kuimarisha usalama nchini sambamba na kulinda maisha ya watu na mali zao.
Aidha, Jeshi la Polisi limeeleza wananchi kuwa picha zinazosambazwa kupitia mitandao ya kijamii kuwa kuna maandamano yameanza si za kweli.
“Taarifa hizo siyo sahihi ni za matukio ya nyuma yakiwepo ya Oktoba 29, 30, 31, 2025. Zingine ni za nyuma zaidi mfano, moja ni tukio la mwezi Juni 2025 ambapo kabila la wamaasai walikuwa na sherehe za jando walizofanyia msitu wa TANAPA Jijini Arusha.
Ikumbukwe kuwa, maandamano yanayopewa jina la maandamano ya amani yalipigwa marufuku toka Disemba 05, 2025 kwani hayakidhi matakwa ya kisheria ikiwepo sheria mama yaani Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na Sheria ya Polisi na Polisi Wasaidizi sura ya 322.
Aidha, tunatoa wito kwa wananchi waendelee kufuata sheria kwa manufaa yetu sote.”
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania