Viongozi wa Kata ya Chanika,wilaya ya Handeni mkoani Tanga wakiongozwa na Diwani wa Kata hiyo, Habibu Mbota, wameunda rasmi Kamati ya Amani ngazi ya kata na mitaa, lengo likiwa ni kusaidia utoaji wa taarifa kuhusu viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.

Mpango huk unatekelezwa kama sehemu ya maelekezo kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, na unalenga kuboresha kamati hizi ili ziweze kutoa ushauri kwa serikali.

Kamati hiyo imekusanya viongozi wa dini mbalimbali, wawakilishi kutoka vyama vya siasa, makundi maalum, wawakilishi wa bodaboda kutoka kila kijiji, pamoja na wazee mashuhuri.

Mtendaji wa kata hiyo Bahasha Mtundia amesema katika mchakato wa uundaji wa kamati hiyo waliwaalika wawakilishi kutoka Polisi Jamii wa Wilaya pamoja na Polisi Kata, wakiungana na wenyeviti wa mitaa lengo ni kuendelea kuimarisha amani na utulivu katika maeneo Yao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *