
Chama cha ANC, kilichoanzishwa na Nelson Mandela, nchini Afrika Kusini kimehitimishaMkutano wake Mkuu (Desemba 8-12) huko Johannesburg, mkutano wa kawaida unawwezesha chama hicho kutathmini hali yake. Zaidi ya kupungua kwa umaarufu ambao kumekilazimisha, tangu Juni 2024, kutawala kwa muungano kwa mara ya kwanza katika miaka thelathini, kimsingi ni matatizo ya kifedha yanayojirudia ya chama hicho yanayotia wasiwasi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Johannesburg, Claire Bargelès
Nchini Afrika Kusini, mkutano huo ulifunguliwa mwanzoni mwa wiki kwa maandamano ya wafanyakazi wa ANC ambao hawajalipwa kwa wiki kadhaa. Katibu mkuu wa chama hicho, Fikile Mbalula, aliwahakikishia kwamba hali hiyo “itatatuliwa hivi karibuni,” huku akikiri kuwepo kwa matatizo ya kifedha ya kimuundo.
“Changamoto kubwa zaidi tutakayoshughulikia baada ya Mkutano huu Mkuu ni suala la uendelevu wetu wa kifedha,” alielezea. “Chama muhimu kama ANC hakiwezi kumudu kuwa na matatizo kama hayo yanayojirudia.”
Chama ambacho kimeishi kwa muda mrefu “zaidi ya uwezo wake”
Ripoti ya fedha haijawekwa wazi. Hata hivyo, baadhi ya takwimu zimetolewa: ANC inatumia zaidi ya euro milioni moja kwa mwezi kwa mishahara. Kampuni moja pia ilielezea mahakamani jinsi ambavyo haikulipwa kikamilifu kwa huduma zilizotolewa.
Kwa mujibu wa mchambuzi wa masuala ya siasa Sandile Swana, matatizo haya yanatokana hasa na njia ya kihistoria ya chama: “Kwa muda mrefu sana, chama kiliishi zaidi ya uwezo wake. Lakini sasa, mfumo wa kisheria ni mkali zaidi, kwa hivyo haiwezekani tena kufikia njia mbalimbali haramu.”
Kwa upande wake, ANC inapinga sheria ya Afrika Kusini inayowataka wafadhili wa zaidi ya euro 5,000 (randi 100,000) kufichua utambulisho wao.