Serikali yaagiza wananchi kuweka akiba ya chakulaSerikali yaagiza wananchi kuweka akiba ya chakula

DODOMA; WAZIRI Mkuu, Dk Mwigulu Nchemba amewataka Watanzania watunze akiba ya chakula walichonacho na waepuke matumizi yasiyofaa kutokana na hali ya kuchelewa kwa msimu wa mvua.

Dk Nchemba alitoa wito huo jana wakati akizungumza na baadhi ya wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya ofisini kwake Mlimwa, jijini Dodoma.

Aliwaeleza viongozi hao kutoka mikoa ya Dodoma na Singida kwamba Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) ilitoa utabiri wa mwelekeo wa msimu wa mvua za vuli na mvua za msimu kwa kipindi cha Oktoba 2025 hadi Desemba 2025 na kipindi cha mwezi Novemba, 2025 hadi Aprili 2026 mtawalia.

“Kutokana na utabiri huo, baadhi ya mikoa nchini inatarajiwa kuwa na mvua za chini ya wastani hadi wastani na kutawaliwa na vipindi virefu vya ukavu na mtawanyiko wa mvua usioridhisha,” alisema

Alisema tathmini hiyo ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania inaonesha hali ya kuchelewa kwa mvua inatara jiwa katika maeneo ya mikoa ya Dodo ma, Katavi, Kigoma, Singida, Tabora, Iringa, Mbeya, Mtwara, Njombe, Songwe, Rukwa, Ruvuma pamoja na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro.

“Pamoja na kuwa hakuna tishio la uhaba wa chakula kutokana na hifadhi ya chakula iliyopo nchini, lakini ni vema, wananchi waendelee kuz ingatia matumizi sahihi ya chakula. Tuna akiba ya chakula ya kutosha lakini ninawasihi wananchi waweke akiba na kuepuka matumizi yasiyo ya lazima,” alisema.

Alitumia fursa hiyo kuwakumbusha wakulima waandae mashamba kwa wakati na watumie pembejeo zinazoendana na upatikanaji wa mvua chache sambamba na kuzingatia ushauri wa wataalamu wa kilimo ambao kwa sasa wanazunguka nchi nzima kukutana na wakulima na kutoa elimu.

Vilevile, Dk Mwigulu aliwataka wafugaji wote waweke mipango mizuri ya matumizi na uhifadhi wa maji na vyakula vya mifugo ili kuk abiliana na hali hiyo.

Alisisitiza pia wakuu wa mikoa na wilaya wahakikishe maofisa ugani wanawatembelea wakulima na kutoa ushauri ikiwemo matumizi sahihi ya mbegu kulingana na hali ya hewa badala ya kukaa ofisini muda wote.

“Vilevile, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri endeleeni kuhamasisha wakulima wajisajili kwenye daftari la mkulima na kuhakikisha wanapata namba za usajili,” alisisitiza.

Aliwataka pia viongozi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC) zihakikishe kuwa shehena za pembejeo zinahudumiwa kwa wakati ili usambazaji ufanyike kwa ufanisi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *