
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Félix Tshisekedi, yuko Luanda, Angola, tangu Jumapili, Desemba 14, kwa ziara ya kikazi, kulingana na vyanzo kadhaa.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kuhusu madhumuni ya ziara hii, baadhi ya vyanzo vinasema kwamba amejitolea kufufua mchakato wa Luanda, mpango wa kidiplomasia unaolenga kurejesha amani mashariki mwa DRC.
Kulingana na Gazeti la LePotentiel, ziara hii inalenga kuimarisha juhudi za upatanishi wa kikanda katika kukabiliana na vurugu zinazoendelea Kivu, hasa zile zinazohusiana na kundi lenye silaha la M23.
Vyanzo vingine vinaripoti kwamba, Mkuu wa Nchi wa Kongo alikutana na mwenzake wa Angola, João Lourenço, kujadili masuala yenye maslahi ya pamoja. Haya ni pamoja na kuimarisha ushirikiano wa pande mbili kati ya DRC na Angola, pamoja na changamoto za kikanda zinazohusiana na amani na usalama katika Afrika ya Kati.
Kwa vyovyote vile, ziara hii inakuja siku chache tu baada ya kuidhinishwa kwa makubaliano ya amani kati ya DRC na Rwanda mnamo Desemba 4, 2025, huko Washington, D.C., chini ya upatanishi wa Marekani. Licha ya makubaliano haya, vita vinazidi kupamba moto katika uwanja wa vita. Waasii wa AFC-M23, wanaoungwa mkono na Kigali, wameteka miji kadhaa huko Kivu Kusini, ikiwa ni pamoja na mji wa kimkakati wa Uvira.