Waendesha mashtaka katika mahakama ya Kimataifa ya ICC, siku ya Jumanne, walianza kuwasilisha ushahidi dhidi ya kiongozi wa kundi la LRA Joseph Kony asiyefahamika alipo, ambaye wapiganaji wake walisababisha mauaji makubwa na mateso kwa waakazi wa Kaskazini mwa Uganda.

Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Waendesha mashtaka wamewaambia na kuwaonesha majaji wanaosikiliza kesi hiyo jijini Hague, namna Joseph Kony na kundi lake wamesababisha maumivu na hofu miongoni mwa watu, na kuwasababishia uoga mpaka sasa.

Wakili anayewawakilisha wahasiriwa Sarah Pellet wemeka bayana mateso waliyoyapitia raia wa Uganda ambapo Kony anakabiliwa na mashtaka 39 ya uhalifu wa kivita na dhulma dhidi ya binadamu.

Joseph Kony- Kiongozi wa kundi la LRA nchini Uganda.
Joseph Kony- Kiongozi wa kundi la LRA nchini Uganda. © AP

Kundi la LRA lilianzisha mashambulizi nchini Uganda katika miaka ya 1980, wakati Kony akijaribu kupindua Serikali iliyo madarakani.

Licha ya kundi lake kuondolewa nchini humo, kundi lake lilienda kutekeleza uhalifu katika vijiji vya Jamuhuri ya Afrika ya Kati, DRC, Sudan Kusini Sudan, ambapo alifahamika kwa kusajili watoto kama wapiganaji.

Kesi yake ya kuthibitisha mashtaka imeanza kusikilizwa miaka kadhaa kupita tangu mahakama hiyo, mwaka 2020 imuhukumu kifungo cha miaka 25 jela Dominic Ongwen, aliyekuwa kamanda wa juu wa kundi la LRA na mtu wa karibu wa Kony, ambapo alichukuliwa akiwa mtoto.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *