
Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki, Hakan Fidan, atafanya ziara rasmi nchini Italia tarehe 11-12 Septemba, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki siku ya Jumatano.
Katika ziara hiyo, Fidan anatarajiwa kukutana na Naibu Waziri Mkuu wa Italia na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Antonio Tajani. Mawaziri hao wawili walikutana mara ya mwisho mjini Antalya pembezoni mwa Mkutano Usio Rasmi wa Mawaziri wa Mambo ya Nje wa NATO uliofanyika Mei 14-15.
Ziara hii inafuatia mfululizo wa mawasiliano ya ngazi ya juu kati ya nchi hizo mbili. Mnamo Aprili 29, jiji la Rome lilikuwa mwenyeji wa Mkutano wa Nne wa Serikali za Uturuki na Italia, ukiongozwa kwa pamoja na Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni. Hivi karibuni zaidi, mnamo Agosti 1, Istanbul mwenyeji wa Mkutano wa Viongozi wa Uturuki-Italia-Libya, ukiongozwa na Rais Erdogan.
Mbali na mazungumzo ya kikazi, Fidan pia anatarajiwa kutoa hotuba inayozunumzia sera katika taasisi ya Istituto Affari Internazionali, moja ya vituo vinavyoongoza kwa tafiti za kisera nchini Italia.
Kwa mujibu wa taarifa ya wizara, mazungumzo kati ya Fidan na Tajani yataangazia ushirikiano wa kimkakati na ushirikiano wao ndani ya muungano wa NATO, umuhimu wa ziara za ngazi ya juu za pande zote, pamoja na lengo la kufikia dola bilioni 40 za biashara kati ya mataifa hayo mawili.
Ankara pia itasisitiza umuhimu wa kusasisha Muungano wa Forodha kati ya Uturuki na Umoja wa Ulaya, na kuangazia fursa za ushirikiano katika usalama wa nishati, miundombinu ya usafirishaji, na sekta ya ulinzi.
Ajenda pia inajumuisha ushirikiano katika kushughulikia uhamiaji usio wa kawaida, uvumbuzi wa kisayansi na kiteknolojia, masuala yanayohusiana na NATO, na uhusiano kati ya Uturuki na Umoja wa Ulaya.
Pande zote pia zinatarajiwa kubadilishana maoni kuhusu masuala ya Libya, Ukanda wa Gaza nchini Palestina, Syria, Ukraine, Iran, na bara la Afrika.