Mwigulu aagiza watumishi Temesa wafutwe kaziMwigulu aagiza watumishi Temesa wafutwe kazi

DAR ES SAALM; WAZIRI Mkuu Dk Mwigulu Nchemba, ameagiza watumishi wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa) waliohusika na ubadhirifu wa fedha kiasi cha Sh bilioni 2.5 wafukuzwe kazi mara moja, akisisitiza kuwa serikali haitavumilia matumizi mabaya ya madaraka na fedha za umma.

Dk Mwigulu ametoa agizo hilo leo Desemba 24, 2025 alipofanya ziara ya kukagua utendaji kazi wa kivuko eneo la Kigamboni, Dar es Salaam, ambapo ameeleza kuwa vitendo vya ubadhirifu vimekuwa chanzo cha kudorora kwa huduma za usafiri wa vivuko na kuongeza gharama zisizo za lazima kwa serikali.

“Watu wasioweza kujirekebisha ni lazima warekebishwe. Kumekuwepo na matumizi mabaya ya madaraka na fedha, hali ambayo haiwezi kuvumiliwa,” amesema Dk Mwigulu.

Amebainisha kuwa kwa sasa matengenezo yamesimama kwa baadhi ya vivuko kutokana na madeni ya takribani Sh milioni 800, huku taarifa za kifedha zikionesha baadhi ya watumishi wa TEMESA wamehusika na ubadhirifu wa Sh bilioni 2.5.

Dk. Mwigulu ameonya kuwa endapo hatua kali hazitachukuliwa, serikali inaweza kujikuta ikitumia fedha nyingi katika matengenezo ya vivuko chakavu badala ya kununua vivuko vipya, hali itakayoongeza mzigo kwa wananchi na kuathiri utoaji wa huduma.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *