#HABARI: Hali ya taharuki imetanda katika Kata za Malolo na Mwinyi ndani ya Manispaa ya Tabora baada ya nyumba zaidi ya 100 kuzingirwa na maji kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kwa takribani saa nne leo. Mvua hiyo imesababisha adha kubwa kwa wakazi wa maeneo hayo, huku mali nyingi zikiharibiwa na miundombinu ya makazi kuathiriwa na mafuriko hayo.
Kufuatia hali hiyo, wananchi wameaswa kuchukua tahadhari za kiusalama na kuhama katika maeneo yenye hatari zaidi wakati jitihada za uokozi na tathmini ya uharibifu zikiendelea kufanywa na mamlaka husika.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.