#HABARI: Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linamshikilia mwananchi mmoja kwa tuhuma za mauaji yaliyotokea wilayani Kilosa baada ya ugomvi unaodaiwa kuchochewa na wivu wa kimapenzi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Rashid Hussein Paulo (35) mkulima na mkazi wa Msowero, ambaye anatuhumiwa kumuua Steven Elia Mayungu (26) mkulima na mkazi wa Mayungu.

Tukio hilo liliripotiwa kutokea Disemba 26, 2025 majira ya saa tano usiku katika Kitongoji cha Shuleni, Kijiji na Kata ya Lumuma, Wilaya ya Kilosa, ambapo wilayani Kilosa ambapo uchunguzi wa awali umebaini marehemu alichomwa kwa kitu chenye ncha kali katika eneo la kifua baada ya kuibuka ugomvi kati yake na mtuhumiwa.

Kamanda Mkama amesema mtuhumiwa anashikiliwa kwa mahojiano zaidi na hatua za kisheria zinaendelea, huku akitoa wito kwa jamii kutatua migogoro ya kifamilia kwa njia ya amani na kufikisha masuala yao kwenye vyombo vya Dola badala ya kujichukulia Sheria mkononi.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *