#HABARI: Tume ya Kuchunguza Matukio ya Uvunjifu wa Amani yaliyojitokeza wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu, leo Disemba 30, 2025, imekutana na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi (CDF), Jenerali Jacob Mkunda.

Kikao hicho ni muendelezo wa majadiliano kati ya tume, waathirika wa matukio ya ghasia wakati na baada ya uchaguzi pamoja na wadau wengine wanaohusika.

Majadiliano hayo yamefanyika kufuatia umuhimu wa nafasi ya Mkuu wa Majeshi, changamoto zilizojitokeza na namna uzoefu wake unavyoweza kusaidia kazi ya tume katika mchakato wa sasa wa uchunguzi.

Tume hiyo inaendelea na majadiliano na wadau mbalimbali kwa lengo la kubaini sababu za msingi zilizosababisha matukio hayo na kupendekeza hatua za kitaifa zitakazosaidia kuzuia matukio kama hayo yasijirudie tena.

Powered by #MCHEZOSUPA

JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:

Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.

#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *