Msanii wa Bongo Fleva na dancer @chino_kidd7 amefunguka kuhusu mambo muhimu ambayo vijana wanapaswa kuyazingatia ili kufanikiwa kwenye fani ya dancing.
Akizungumza kupitia TheSpark ya Clouds TV, Chino amesema mafanikio ni mchakato na sio jambo la haraka. Ameeleza kuwa ni lazima kijana ajitoe kikamilifu, kwani hata yeye alianza kwa kufanya show za bure. Pia amesisitiza kuwa hata wasanii huanza kwa kutumbuiza bila malipo ili kujenga majina yao kabla ya muziki kugeuka kuwa biashara.
Cc: @missloloh_ @djfantastic255
#TheSparkShow
#Clouds26Nyoosha